Book Description
Wakizingatia historia ndefu ya uandishi katika lugha ya Kiswahili, majaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasihi ya Afrika wameeleza: Mashairi yaliyomo katika diwani hii yametumiliwa lugha iliyojaa taswira na majazanda yanayowakilisha vyema hisia zinazoelezwa katika dhamira mbalimbali. Mshairi amefaulu sana kuzitumia mbinu na miundo kadha wa kadha ili kuyajadili maswala yanayohusu hali na mazingira tafauti tafauti katika maisha ya binadamu. Anayazungumza maswala mazito mazito, lakini kwa namna ambayo hayamuelemei msomaji wake. Bali, badala yake, huwa yanamhimiza aendelee kuyasoma. Hata yale maswala makongwe, kwa mfano uhusiano baina ya wazazi na wana wao, yanajadiliwa kwa namna ya kuvutia na kuyafanya kama kwamba ndiyo mwanzo yanaanza kujadiliwa sasa. Dotto Rangimoto ni mtunzi stadi. Na diwani hii ni mchango mkubwa katika ushairi wa Kiswahili wa zama zetu hizi.